Tutakusaidia kuandaa mkakati ambao utautumia
kama mwongozo kwa ajili ya kufanikisha malengo ya blog yako. Kazi ya pakeji hii
ni kusaidia kukupa fursa kubwa zaidi ya kufanikiwa kwa kufanya yafuatayo (i) Tunachukua malengo unayotaka kufikia na
blog yako (ii) Kuyatafsiri na kutengeneza mkakati utakao kuwezesha kufikia
malengo yako iwe ni mtu binafsi, biashara, kampuni, NGO n.k.
Huduma utakazopata ni pamoja na:
- Kutengeneza mkakati wa blogu yako ambao utahusisha maudhui, muundo pamoja na usimamizi wa blogu yako.
- Kujua ni rasilimali zipi utahitaji (watu, fedha n.k.) kufanikisha malengo yako
- Kukusaidia kuchagua zana zitakazo kusaidia kuendesha blog yako kwa urahisi zaidi
- Kukupa muhtasari wa maeneo yanayo hitaji mafunzo kusaidia uendeshaji mzuri wa blogu
- Kubaini vigezo vya mafanikio vitakavyo kuwezesha kupima mafanikio ya blogu yako siku ha siku.