Social Media (Swahili)

Matumizi na umaarufu wa mitandao ya jamii na ushawishi wake unazidi kuongezeka mtandaoni siku hadi siku. Kwa Tanzania mitandao ya Facebook na Twitter imekuwa ni sehemu muhimu ya maisha ya watumiaji wengi wa mtandao. Yote haya yameifanya mitandao ya jamii kuwa kiungo muhimu kinacho changia ongezeko la watu wanaotembelea blogu. Pakeji hii itaiwezesha blogu yako na makala zake kufikia watu wengi zaidi kwa kuitumia mitandao ya jamii.

Tutaunganisha blogu yako na hadi mitandao mitatu muhimu ya jamii (facebook,twitter, linkedin n.k) ambayo inatumiwa aina ya watu unaotaka watembelee blogu yako. Tutatengeneza kurasa za mitandao yako yote ya jamii na kukupa muongozo wa namna ya kuitumia kwa ufanisi zaidi.

Huduma utakazopata ni pamoja na
  • Usajili wa akaunti za hadi mitandao mitatu ya jamii pamoja na kutengeneza kurasa zake.
  • Kuunganisha mitandao yako ya jamii na blogu yako.
  • Kukupatia vifaa vitakavyokuwezesha kuendesha na kusimamia mitandao yako ya jamii kwa urahasi.
Pakeji hii inaanzia TZS 1OO,OOO.oo kwa kila mtandao wa kijamii (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)