Branding Package (Swahili)

Ukiona alama ya tiki kwenye kiatu huhitaji kuona jina kujia kwamba ni kiatu cha Nike. Mabasi ya Abood au Dar Express, chupa ya Konyagi n.k. huhitaji kuona majina yake kuzitambua. Haya yota ni matokeo ya branding, iwe kwa makusudi au bahati. Kwa kutumia rangi (Abood, Precision), nembo (Nike, Vodacom) au umbo la bidhaa (Konyagi) branding imewezesha bidhaa na huduma nilizozitaja hapo juu kujitofautisha na wengine machoni mwa umma.
Japo mafanikio ya brand yanatokana na ubora wa kazi, huduma au bidhaa yako, branding inakuwezesha kujitofautisha na wengine hasa katika muonekano. 

Pakeji hii itakuwezesha blogu yako iweze kutambulika kirahisi kwa kutumia rangi, nembo, kauli mbiu n.k. ambazo zitakuwa za kipekee kwa ajili ya blogu pamoja na mitandao yako ya kijamii.

Vile vile utapata vitu vyote husika kutoka katika pakeji za “Basic”, “Custom”, “Social Media”, “Search Engine Optimization” na “Analytics”.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Branding ya blogu yako kwa kutumia rangi, picha, nembo za kipekee n.k.
  • Branding ya mitandao yako ya kijamii ifanane na branding ya blogu yako
  • Mwongozo pamoja na fasihi zitakazo kukusaidia kutekeleza mikakati ya kukuza brand yako.
Pakeji hii inaanzia TZS 85O,OOO.oo + TZS 8O,OOO.oo kwa kila mtandao wa kijamii  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)