• Start a Blog

    Start a Blog

    Whether it's a personal or business Blog, we can help you get started.

  • Blog Tweaks

    Blog Tweaks

    We help you make small changes to your Blog that make a big difference.

  • Blog Strategy

    Blog Strategy

    We will help you develop a strategy for your Blog's success.

  • Branding

    Branding

    Helping your Blog and Social Media platforms standout from the crowd.

  • Analytics

    Analytics

    Use your Blog visitors' interaction data to improve your Blog.

  • Management

    Management

    Let us manage your Analytics and Webmaster tools so you can focus on blogging.

Showing posts with label wenye blog. Show all posts
Showing posts with label wenye blog. Show all posts

Blog Tweaks (Marekebisho ya Blogu)

Blogu yako inapoendelea kukua umuhimu wa kufanya marekebisho madogo madogo kuboresha au kuendana na ukuaji wa Blogu yako unaongezeka. Kama unataka kufanya marekebisho kwenye Blogu yako basi hii pakeji itakusaidia kutimiza malengo yako.

Tutakusaidia kufanya marekebisho ya kila kitu kuanzia mabango, rangi, picha, jina la Blogu, kuondoa au kuweka vifaa n.k.

Tuambie ni nini unataka kufanya nasi tutakueleza namna tutakavyo weza kukusaidia. 

Pakeji hii inaanzia Shs TZS 2O,OOO.oo (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Analytics (Swahili)

Kama unataka kujua jinsi watu wanaokutembelea wanachofanya wafikapo kwenye blogu yako basi hii pakeji ni kwaajili yako. Pakeji hii itakuwezesha kujua wanaotembelea blogu yako walipotoka, kurasa wanazotembelea, kurasa zinazotembelewa zaidi,muda wanaokaa kwenye blogu yako na mabo mengine mengi. Kwa ufupi pakeji hii itakuwesha kuboresha na kukuza blogu yako kwa kutumia data za wageni wako kuwapa wanachotaka na kuondoa wasichotaka.

Tutaunganisha blogu yako pamoja na mitandao yako ya kijamii na Google Analytics pamoja na kukupa mwongozo wa mambo muhimu yatakayo kuwezesha kutumia Google Analytics kwa ufanisi.

(Kama unataka tukusaidie kusimamia analytics basi ingia hapa)

Huduma utakazo pata ni pamoja na:
  • Kuunganisha blogu yako pamoja na mitandao yako ya jamii na Google Analytics
  • Mwongozo pamoja na fasihi kuhusu vipengele viwili muhimu vya Google Analytics (Trafiki & Maudhui).
Pakeji hii inaanzia TZS 15O,OOO.oo  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Blog Strategy Development (Swahili)

Kuendesha blogu yako siku hadi siku si kazi rahisi na kama hujajipanga vizuri uwezekano wa kushindwa au kukata tamaa na kuacha kublog unaongezeka maradufu. Kama ndiyo kwanza unaanza kublog au tayari unablog unahitaji kuwa na mkakati wa maendeleo kwa ajili ya blog yako. Ukiwa na mkakati madhubuti kwa ajili ya blogu yako, inakusaidia kuweka nguvu zako kwenye mambo ambayo yatasaidia kuiendeleza blogu yako. 

Tutakusaidia kuandaa mkakati ambao utautumia kama mwongozo kwa ajili ya kufanikisha malengo ya blog yako. Kazi ya pakeji hii ni kusaidia kukupa fursa kubwa zaidi ya kufanikiwa kwa kufanya yafuatayo  (i) Tunachukua malengo unayotaka kufikia na blog yako (ii) Kuyatafsiri na kutengeneza mkakati utakao kuwezesha kufikia malengo yako iwe ni mtu binafsi, biashara, kampuni, NGO n.k.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Kutengeneza mkakati wa blogu yako ambao utahusisha maudhui, muundo pamoja na usimamizi wa blogu yako.
  • Kujua ni rasilimali zipi utahitaji (watu, fedha n.k.) kufanikisha malengo yako
  • Kukusaidia kuchagua zana zitakazo kusaidia kuendesha blog yako kwa urahisi zaidi
  • Kukupa muhtasari wa maeneo yanayo hitaji mafunzo kusaidia uendeshaji mzuri wa blogu
  • Kubaini vigezo vya mafanikio vitakavyo kuwezesha kupima mafanikio ya blogu yako siku ha siku.
Pakeji hii inaanzia TZS 35O,OOO.oo  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Branding (Swahili)

Ukiona alama ya tiki kwenye kiatu huhitaji kuona jina kujia kwamba ni kiatu cha Nike, vivyo hivyo kwa bidhaa na huduma za Bakhresa. Mabasi ya Abood au Dar Express, chupa ya Konyagi n.k. huhitaji kuona majina kuzitambua. Haya yota ni matokeo ya branding, iwe kwa makusudi au bahati, kwa kutumia rangi (Abood, Precision), nembo (Nike, Vodacom) au umbo la bidhaa (Konyagi) branding ndiyo imewesha bidhaa na huduma nilizozitaja hapo juu kujitofautisha na wengine machoni mwa umma.

Japo mafanikio ya brand yanatokana ubora wa kazi, huduma au bidhaa yako, branding inawesha watu kutambua blogu yako kutoka kwenye utitiri wa blogu mtandaoni. Pakeji hii itawezesha blogu yako iweze kutambulika kirahisi kwa kutumia rangi, nembo, slogan n.k. ambazo zitakuwa za kipekee kwaajili ya blogu pamoja na mitandao yako ya kijamii.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Branding ya blogu yako kwa kutumia rangi, picha, nembo za kipekee n.k.
  • Branding ya mitandao yako ya kijamii ifanane na branding ya blogu yako
  • Links na resources za kukusaidia kutekeleza mikakati yako ya kukuza brand yako.
Pakeji hii inaanzia TZS 25O,OOO.oo + TZS 1OO,OOO.oo kwa kila mtandao wa jamii   (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Custom Template (Swahili)

Zile zama za kuanzisha blogu kwa kutumia tamplate ya blogger, kuanza kublogu na kutegemea utapata traffic zimeisha. Pamoja na kuwa na maudhui mazuri, template iliyo undwa vizuri utakayo wezesha watu kutumia blogu yako kirahisi ni muhimu. Custom template inafanya kazi kwa ajili ya blogu yako badala ya kulazimisha blogu yako kufuata muongozo wa template.

Template ni kama nguo, kila nguo inamahali pake na vile vile nguo hupitwa na wakati kwa hiyo template nazo zinahitaji kubadilika na kuendana na ukuaji na mahitaji mapya ya blogu yako.

Pakeji hii itakusaidia kufunga custom template ambayo itawezesha blogu yako kufanya kazi unavyo taka na kuwana mvuto zaidi.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Tutakusaidia kuchagua, kuinstall na kucustomize template itakayo kidhi mahitaji yako.
  • Tutainstall widgets na plug ins kusaidia blogu yako ifanye kazi vizuri.
  • Tutakufungulia akaunti ya Flickr kwaajili ya kuhifadhi picha za template yako.
  • Tutakupa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi yak u hifadhi picha za template yako.
  • Tunaweza kukusaidia kuunganisha domain name kwenye blogu yako (Kwagharama ya ziada)
Pakeji hii inaanzia TZS 25O,OOO.oo (kwa Blogu mpya) & TZS 3OO,OOO.oo (Blogu za zamani) (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Search Engine Optimization SEO (Swahili)

Zaidi ya 50% ya watu wote wanaotumia mtandao duniani hutumia search engines (Google, Bing n.k.) kutafuta watakacho mtandaoni. Kurekebisha blogu yako kwa ajili ya search engines kunaiwezesha blogu yako kunufaika zaidi na umati unaotumia search engines. Pakeji hii itawezesha search engines kuweza kupitia makala zako na kuhifadhi maudhui yake kwa ajili ya watumiaji wake (mfano mtu anapotafuta kitu kinachoshabihiana na maudhui ya makala zako, search engine zitampa kurasa za blogu yako kwenye majibu yake). 

Tutarekebisha blogu yako kwa ajili ya search engine 3 bora kwa idadi ya watumiaji (Google, Bing & Yahoo). Pia tutaunganisha blogu yako na vyombo vitakavyo kuwezesha kufuatilia na kusimamia utendaji wa blogu yako kwenye search engines.

(Kama unataka tusimamie vyombo vya SEO yako basi ingia hapa)

Huduma utakazozipata ni pamoja na :

Kurekebisha blogu yako kwa ajili ya SEO, na hii itahusisha pamoja na mambo mengine
  • Tags [meta and description], images etc
  •  Link optimization [back links, no follow, do follow, no index etc]
Kuunganisha blogu yako na webmaster tools pamoja na
  •  Kurekebisha blogu yako kutumia webmaster tools
  • Kutuma ramani ya blogu yako kwenda kwenye search engines
  • Mwongozo wa jinsi ya kutumia vipengele muhimu vya Webmaster Tools
Pakeji hii inaanzia TZS 25O,OOO.oo (Kwa blogu mpya) & TZS 4OO,OOO.oo (Blogu za zamani)   (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Social Media (Swahili)

Matumizi na umaarufu wa mitandao ya jamii na ushawishi wake unazidi kuongezeka mtandaoni siku hadi siku. Kwa Tanzania mitandao ya Facebook na Twitter imekuwa ni sehemu muhimu ya maisha ya watumiaji wengi wa mtandao. Yote haya yameifanya mitandao ya jamii kuwa kiungo muhimu kinacho changia ongezeko la watu wanaotembelea blogu. Pakeji hii itaiwezesha blogu yako na makala zake kufikia watu wengi zaidi kwa kuitumia mitandao ya jamii.

Tutaunganisha blogu yako na hadi mitandao mitatu muhimu ya jamii (facebook,twitter, linkedin n.k) ambayo inatumiwa aina ya watu unaotaka watembelee blogu yako. Tutatengeneza kurasa za mitandao yako yote ya jamii na kukupa muongozo wa namna ya kuitumia kwa ufanisi zaidi.

Huduma utakazopata ni pamoja na
  • Usajili wa akaunti za hadi mitandao mitatu ya jamii pamoja na kutengeneza kurasa zake.
  • Kuunganisha mitandao yako ya jamii na blogu yako.
  • Kukupatia vifaa vitakavyokuwezesha kuendesha na kusimamia mitandao yako ya jamii kwa urahasi.
Pakeji hii inaanzia TZS 1OO,OOO.oo kwa kila mtandao wa kijamii (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more