• Start a Blog

    Start a Blog

    Whether it's a personal or business Blog, we can help you get started.

  • Blog Tweaks

    Blog Tweaks

    We help you make small changes to your Blog that make a big difference.

  • Blog Strategy

    Blog Strategy

    We will help you develop a strategy for your Blog's success.

  • Branding

    Branding

    Helping your Blog and Social Media platforms standout from the crowd.

  • Analytics

    Analytics

    Use your Blog visitors' interaction data to improve your Blog.

  • Management

    Management

    Let us manage your Analytics and Webmaster tools so you can focus on blogging.

Showing posts with label Anzisha Blog. Show all posts
Showing posts with label Anzisha Blog. Show all posts

Basic Package (Swahili)

Kama ndiyo unataka kuanzisha blogu na unachohitaji ni blogu ya kawaida itakayo kuwezesha kuanza kublogua mara moja, hii ni sehemu nzuri ya kuanzia. Kwenye pakeji hii tutakusaidia kuanzisha blogu yako tayari kwa wewe kuanza kublog na pia utapata muongozo wa namna yakuandika nakala yako ya kwanza.  

Huduma utakazo pata ni pamoja na:
  • Kusajili akaunti yako ya Google
  • Tutakusaidia kuchagua majina matatu ambapo moja wapo litatumika kama jina la blogu yako
  • Tutakusaidia kutengeneza kichwa cha blog (title) ambayo itasaidia kulezea kuhusu blogu yako
  • Kufunga template ya chaguo lako kutoka Blogger
  • Kutekeleza mapendekezo yako katika mambo yafuatayo
            Waandishi - Nani atakuwa na ruhusa ya kuandika, kusahihisha n.k.
                   Maoni - Nani anaweza kuacha maoni
                 Makala - Ni namna gani makala zako zitaoneka
  • Muongozo wa namna ya kuandika makala yako ya kwanza, picha, video n.k.
Gharama ya Pakeji hii ni TZS 1OO,OOO.oo (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Custom Package (Swahili)

Zile zama za kuanzisha blogu na kutegemea watu watembelea blogu yako zinafikia ukingoni. Pamoja na nakala zenye maudhui yenye mvuto, template iliyokarabatiwa kusaidia blogu yako kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ni muhimu. Template ya kawaida inailazimu blogu yako kufanya kazi kwa kufuata matakwa yake badala ya matakwa yako na ya maudhui ya blogu yako.
Template ni kama nguo, kila nguo inamahali na wakati wake, vile vile nguo hupitwa na wakati au kuchakaa. Kama nguo template nazo zinahitaji kuendana na mahitaji ya blogu yako (mfano kama unablogu ya mitindo, unahitaji template inayo kuwezesha kuonyesha mitindo mbali mbali kwa urahisi).
Kwenye pakeji hii tutakufungia template iliyo karabatiwa kukidhi mahitaji yako itakayo wezesha blogu yako kufanya kazi unavyo taka na kuwana mvuto zaidi.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Tutakusaidia kuchagua, kufunga na kukarabati template itakayo kidhi mahitaji yako.
  • Tutakufungulia akaunti ya Flickr kwaajili ya kuhifadhi picha za template yako.
  • Tutakupa mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuhifadhi picha za template yako.
  • Tunaweza kukusaidia kuunganisha domain name kwenye blogu yako (Kwagharama ya ziada)
Pakeji hii inaanzia TZS 3OO,OOO.oo  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Social Media Package (Swahili)

Matumizi na umaarufu wa mitandao ya jamii na ushawishi wake unazidi kuongezeka mtandaoni siku hadi siku. Kwa Tanzania mitandao ya Facebook na Twitter imekuwa ni sehemu muhimu ya maisha ya watumiaji wengi wa mtandao. Yote haya yameifanya mitandao ya jamii kuwa kiungo muhimu kinacho changia ongezeko la watu wanaotembelea blogu. Pakeji hii itaiwezesha blogu yako na makala zake kufikia watu wengi zaidi kwa kuitumia mitandao ya jamii.


Tutaunganisha blogu yako na hadi mitandao mitatu muhimu ya jamii (facebook,twitter, linkedin n.k) ambayo inatumiwa aina ya watu unaotaka watembelee blogu yako. Tutatengeneza kurasa za mitandao yako yote ya jamii na kukupa muongozo wa namna ya kuitumia kwa ufanisi zaidi.

Vile vile utapata vitu vyote husika kutoka katika pakeji ya Basic na Custom. (Kama unachohitaji ni kuunganisha blogu yako na mitandao ya jamii peke yake basi ingia hapa)

 Huduma utakazopata ni pamoja na
  • Usajili wa akaunti za hadi mitandao mitatu ya jamii pamoja na kutengeneza kurasa zake.
  • Kuunganisha mitandao yako ya jamii na blogu yako.
  • Kukupatia vifaa vitakavyokuwezesha kuendesha na kusimamia mitandao yako ya jamii kwa urahasi.
Pakeji hii inaanzia TZS 45O,OOO.oo  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Search Engine Optimization SEO Package (Swahili)

Zaidi ya 50% ya watu wote wanaotumia mtandao duniani hutumia search engines (Google, Bing n.k.) kutafuta watakacho mtandaoni. Kurekebisha blogu yako kwa ajili ya search engines kunaiwezesha blogu yako kunufaika zaidi na umati unaotumia search engines. Pakeji hii itawezesha search engines kuweza kupitia makala zako na kuhifadhi maudhui yake kwa ajili ya watumiaji wake (mfano mtu anapotafuta kitu kinachoshabihiana na maudhui ya makala zako, search engine zitampa kurasa za blogu yako kwenye majibu yake).  


Tutarekebisha blogu yako kwa ajili ya search engine 3 bora kwa idadi ya watumiaji (Google, Bing & Yahoo). Pia tutaunganisha blogu yako na vyombo vitakavyo kuwezesha kufuatilia na kusimamia utendaji wa blogu yako kwenye search engines.

Vile vile utapata kila kitu kinacho husika kutoka katika pakeji za “Basic”, “Custom” na “Social Media”. 

(Kama unataka tusimamie vyombo vya SEO yako basi ingia hapa)

Huduma utakazozipata ni pamoja na :

Kurekebisha blogu yako kwa ajili ya SEO, na hii itahusisha pamoja na mambo mengine
  • Tags [meta and description], images etc
  • Link optimization [back links, no follow, do follow, no index etc]
Kuunganisha blogu yako na webmaster tools pamoja na
  • Kurekebisha blogu yako kutumia webmaster tools
  • Kutuma ramani ya blogu yako kwenda kwenye search engines
  • Mwongozo wa jinsi ya kutumia vipengele muhimu vya Webmaster Tools
Pakeji hii inaanzia TZS 6OO,OOO.oo (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Analytics Package (Swahili)

Kama unataka kujua wanachofanya watu wanaokutembea blogu yako basi hii pakeji ni kwaajili yako. Pakeji hii itakuwezesha kujua wanaotembelea blogu yako walipotoka, kurasa na makala wanazotembelea, kurasa zinazotembelewa zaidi,muda wanaokaa kwenye blogu yako na mambo mengine mengi. Kwa ufupi pakeji hii itakuwesha kuboresha na kukuza blogu yako kwa kutumia tabia za wageni wako kuwapa wanachotaka. Google Analytics ndiyo chombo kinatakacho kuwezesha kupata data zote hizi.

Tutaunganisha blogu pamoja na mitandao yako ya kijamii na Google Analytics pamoja na kukupa mwongozo wa mambo muhimu yatakayo kuwezesha kutumia Google Analytics kwa ufanisi.

Vile vile utapata mambo yote husika kutoka katika pakeji za  “Basic”, “Custom”, “SocialMedia” na “SEO”. 

(Kama unataka tukusaidie kuisimamia Google Analytics basi ingia hapa)

Huduma utakazo pata ni pamoja na:
  • Kuunganisha blogu pamoja na mitandao yako ya jamii na Google Analytics
  • Mwongozo pamoja na fasihi kuhusu vipengele viwili muhimu vya Google Analytics (Trafiki & Maudhui).
Pakeji hii inaanzia TZS 75O,OOO.oo  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more

Branding Package (Swahili)

Ukiona alama ya tiki kwenye kiatu huhitaji kuona jina kujia kwamba ni kiatu cha Nike. Mabasi ya Abood au Dar Express, chupa ya Konyagi n.k. huhitaji kuona majina yake kuzitambua. Haya yota ni matokeo ya branding, iwe kwa makusudi au bahati. Kwa kutumia rangi (Abood, Precision), nembo (Nike, Vodacom) au umbo la bidhaa (Konyagi) branding imewezesha bidhaa na huduma nilizozitaja hapo juu kujitofautisha na wengine machoni mwa umma.
Japo mafanikio ya brand yanatokana na ubora wa kazi, huduma au bidhaa yako, branding inakuwezesha kujitofautisha na wengine hasa katika muonekano. 

Pakeji hii itakuwezesha blogu yako iweze kutambulika kirahisi kwa kutumia rangi, nembo, kauli mbiu n.k. ambazo zitakuwa za kipekee kwa ajili ya blogu pamoja na mitandao yako ya kijamii.

Vile vile utapata vitu vyote husika kutoka katika pakeji za “Basic”, “Custom”, “Social Media”, “Search Engine Optimization” na “Analytics”.

Huduma utakazopata ni pamoja na:
  • Branding ya blogu yako kwa kutumia rangi, picha, nembo za kipekee n.k.
  • Branding ya mitandao yako ya kijamii ifanane na branding ya blogu yako
  • Mwongozo pamoja na fasihi zitakazo kukusaidia kutekeleza mikakati ya kukuza brand yako.
Pakeji hii inaanzia TZS 85O,OOO.oo + TZS 8O,OOO.oo kwa kila mtandao wa kijamii  (Ingia HAPA kupata makisio ya gharama BURE)


Read more